Akizungumza na Championi Ijumaa, jana, Okwi ambaye amejiunga na Simba hivi karibuni akitokea Yanga na kusaini kuichezea klabu hiyo kwa miezi sita, amesisitiza kuwa anaipenda Simba na atafanya hivyo pia itakapobidi ili kulinda kiwango chake.
“Unajua sasa hivi nimebadilika na siyo Okwi yule waliyekuwa wakimjua, sitakuwa mtukutu kama ambavyo walikuwa wakinisema mwanzoni,” alisema Okwi.
Mganda huyo ameongeza kuwa anaamini yuko mahali sahihi, hivyo atahakikisha anapambana kuweka kiwango chake kuwa bora. “Nimefurahi kurejea Simba na kuitumikia timu hii, mshahara siyo tatizo,” alisema Okwi.
ConversionConversion EmoticonEmoticon