Tofauti Za Tyga Na Young Money Zimemsukuma Kuendeleza Kazi Zake Na Huyu Mshkaji Wake.

Baada ya mixtape yao ya Fan of a Fan kufanikiwa sana mwaka 2010 sasa Chris Brown na Tyga wamerudi studio kutoa album yao pamoja ya Fan of a Fan iliyotakiwa kutoka 2012.

Tyga ametumia twitter kutufahamisha kuwa wimbo mpya utaitwa “Nothin’ Like Me” Na kashirikishwa Ty Dolla $ign na wimbo umetayarishwa na producer DJ Mustard.

Mwezi wa pili wimbo wa 'Bitches' ulivuja na baadae Chris na Tyga walionekana studio na msanii Boosie Badazz. Album ya Fan Of A Fan itatoka 2015 baada ya kutoka kwa album ya The Gold Album: 18th Dynasty ya Tyga mnamo December 13. 

Tyga  pia ataungana na Chris na Trey Songz kwenye ziara ya 'Between The Sheets' inayoanza January.
Previous
Next Post »