Wema Sepetu hutoza mpaka dola elfu 2 kumuwekea mtu tangazo kwenye akaunti yake ya Instagram

Wema Sepetu Katika Pozi Wakati wengine wanazitumia vibaya akaunti zao za mitandao ya kijamii kutukana na kudhalilisha watu, wapo baadhi ambao wamegundua fursa ana kuzitumia kuingiza pesa.

wema

Mtaji pekee unaohitajika ili uwe katika nafasi nzuri ya kutengeneza pesa kupitia mitandao ya kijamii ni kuwa na followers wengi.

Wema Sepetu ambaye ana followers 483,905 mpaka sasa kwenye akaunti yake ya Instagram amesema kuwa hivi sasa anaitumia akaunti yake kibiashara.

mi naweza kusema kwamba linapokuja swala la utangazaji (wa biashara) imerahisisha kazi Instagram sana, the more followers you got, the more money you make. So kama unataka nipost unanilipa. So imefika hivyo sababu Instagram inatumika sana kwenye matangazo sasa hivi. Mimi nimejua maduka mengine mengi labda ya nguo, accessories hata sehemu mpya za kutengeneza keki kupitia Instagram so what its matangazo.” Wema aliiambia 255 ya XXL ya Clouds Fm.

Ni kiasi gani Wema anatoza kuweka post ya mtu Instagram?

Tunakubaliana nikiiweka post yako ninaiacha kwa muda gani, masaa matano, naiacha siku nzima[…] awe kama na dola elfu moja flani elfu mbili hivi its okay its just a post its not like am appearing on billboard” alimaliza.
Previous
Next Post »