Askofu Pengo akaza uzi, Asema Hawezi Badili Msimamo wake "Waacheni Waumini Wafanye Maamuzi yao Wenyewe Juu ya Kupiga Kura ya Ndio Ama Hapana"

ASKOFU Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Muadhama Polycarp Kardinali Pengo amesema msimamo wake kuhusu Katiba Inayopendekezwa uko pale pale na ametaka wanaoamini alichosema, wasambaze ujumbe wake kwa wengine.

Akizungumza na Chama cha Wanawake Wakatoliki Tanzania (WAWATA) hivi karibuni, Askofu Pengo alitoa wito kwa waumini kuachwa huru wafanye maamuzi yao wenyewe juu ya kuipigia kura ya ndiyo au hapana Katiba Inayopendekezwa badala la kushinikizwa na viongozi wa dini kuipigia kura ya ‘hapana’ katiba hiyo.

Aidha, amesema kamwe hawezi kubadili kile alichosema kwani ni ukweli anaouamini na alishaweka hilo wazi.
Previous
Next Post »