Katika
style kama ile ya shambulizi la Westgate Mall, wanamgambo wa al-Shabaab
wamevamia na kushambulia chuo kikuu cha Garissa kilichopo katika
mji wa Garissa. Zaidi ya watu 15 wameuawa, na wengine zaidi ya 53
wamejeruhiwa.
Mkuu
wa jeshi la polisi Kenya, Inspector General Joseph Boinnet amesema kuwa
magaidi hao walivamia geti kuu la chuo hicho na kuwarushia risasi
walinzi alfajiri saa 5.30, wakati wanafunzi wa Kiislam wakienda kwenye
swala ya asubuhi.
Polisi
waliokuwepo chuoni hapo walikimbilia katika eneo la tukio na kuanza
kurushiana risasi na magaidi hao, ambao walifanikiwa kuingia kwenye
mabweni ya wanafunzi.
Polisi wa ziada na wanajeshi waliitwa kuja kusaidia na mirindimo ya risasi ilisikika kati ya wavamizi hao, polisi na wanajeshi.
Wanafunzi waliokuwa wakipiga simu kutoka ndani ya mabweni wamesema kuwa kuna majeruhi wengi sana.
Wanafunzi
waliofanikiwa kutoroka wamesema kuwa idadi ya wavamizi hao ni angalau
watano na bado kuna wanafunzi na maprofesa wengi wanashikiliwa mateka.
Taarifa za hivi punde zinaarifu kuwa magaidi hao wameanza kuwachinja baadhi ya mateka waliowashikilia.
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ametuma salamu za rambi rambi kwa familia za wale waliouawa katika shambulizi hilo.
Kenyatta amewataka wakenya kuwa watulivu wakati huu ambapo maafisa wa usalama wanakabiliana na wapiganaji hao.
Wanajeshi wa jeshi la Kenya katika geti la chuo hicho |
Baadhi ya miili ya marehemu waliouawa katika shambulio la al-Shabaab katika chuo kikuu cha Garissa |
Helicopter ya jeshi ikitua na maiti na baadhi ya majeruhi katika kambi ya jeshi la Langata |
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Excel, iliopo karibu na chuo kikuu cha Garissa wakiondolewa kutoka shuleni kuhakikisha usalama wao |
ConversionConversion EmoticonEmoticon