Mwigizaji Shamsa Ford, Ney wa Mitego Ndani ya "PENZI ZITO"


Baada ya ivi karibuni staa aliyefanya vizuri kwenye movie ya CHAUSIKU, shamsa ford kutangaza rasmi kuachana na aliyekuwa mume wake, kwa kigezo kuwa mwanaume huyo alikuwa akimtesa na kumpiga kwa muda mrefu, uku akimshutumu mwanaume huyo kutoijali familia yake zaidi ya marafiki na starehe, kitu ambacho kimemfanya staa huyo ajiweke pembeni kuepusha msongamano.
Siku chache baada ya staa huyo kutangaza rasmi kuachana na zilipendwa wake huyo anayefahamika kwa jina moja la dickson, ivi sasa staa huyo yupo kwenye mahaba mazito na mwana hip hop maarufu nchini, ney wa mitego, ambapo kwa nyakati tofauti wameonekana wakiwa wote zero distance , uku wakijiachia na mapicha kama ilivyo kawaida ya mastaa watafuta kick.
Kitendo hicho kimewashtua kama sio kuwapandisha presha wapenda ubuyu wa mujini.
Previous
Next Post »