Chidi Benz kufikishwa mahakamani Leo.


Chidi Benz kufikishwa mahakamani Leo.


Rapper Chidi Benz anatarajiwa kufikishwa mahakamani siku ya leo kujibu mashitaka kutokana na kesi ya kukamatwa na Dawa za Kulevya, tukio lililotokea Ijumaa wiki iliyopita.

Kwa mujibu wa Kamanda Geofrey Nzowa, Mkuu wa Kikosi cha kupambana na dawa za Kulevya nchini, Chidi Benz atafikishwa katika mahakama ya Kisutu ambapo atasomewa mashitaka yake kwa mara ya kwanza.

Chidi alipatikana na dawa za kulevya aina ya Heroine kete zipatazo 14 pamoja na misokoto ya Bangi katika kiwanja cha ndege cha Julius Nyerere akiwa anaelekea Mbeya kwa shughuli za kimuziki.
Previous
Next Post »