Hawa ndio mastaa wanaogombea Ubunge jimbo moja kupitia vyama tofauti.

Red CarpetTaarifa kuhusiana na mastaa mbali mbali ikiwemo wa muziki, filamu, na michezo kuingia katika headline zinazowazungumzia kujihusisha na siasa sio taarifa ngeni kuzisikia, ambapo kwa sasa mastaa wa movie wanaingia kwenye headline nyingine ya wao kwa wao kugombea nafasi ya ubunge kwenye jimbo moja kupitia vyama tofauti.
Mastaa wa filamu kutoka Nigeria Bob Manuel Udokwu na Tony One Week Muonago wanaendelea kuzungumziwa sio kwa sababu wamejiingiza kwenye siasa, bali kinachozungumziwa ni kitendo cha wao kugombea nafasi hiyo katika jimbo moja kitu  ambacho kimeanza kuvutia hisia za watu wengi.
Actors
Bob Manuel Udokwu (kushoto) na Tony One Week, waigizaji wa Nollywood waliojitosa kugombea katika Jimbo la Anambra.
Bob Manuel Udokwu anagombea kupitia chama cha APGA na Tony One Week Muonagor anagombea kwa tiketi ya ACN katika jimbo moja la Anambra, Nigeria ambapo uchaguzi mkuu wa nchi hiyo unatarajiwa kufanyika katikati ya mwaka 2015, ambapo staa mwingine wa Nollywood ambaye alitangaza kujiingiza kugombea ubunge ni Desmond Elliot.
Previous
Next Post »