Tuzo Ya Ballon d'Or 2014,Hawa Wanategemewa Kung'ara.

Mshambuliaji wa Wales Gareth Bale ndio mchezaji pekee kutoka Uingereza kuorodheshwa kati ya wachezaji wanaoshindania tuzo la mchezaji bora  duniani Ballon d’Or huku mshambuliaji wa Real Madrid Christiano Ronaldo akitarajiwa kushinda tuzo hio.
Bale, mwenye umri wa miaka 25, aliweza kuifungia Real Madrid mabao 22 msimu uliopita na kuwezesha Real Madrid kunyakua kombe la klabu bingwa duniani

Lionel Messi ambaye ameshinda taji hilo mara tatu pia yuko miongoni mwa achezaji waliotajwa kwenye orodha hiyo akiwa na mwenzake Neymar
Orodha hiyo ya wachezaji 23 itapunguzwa hadi watatu ambapo mshindi atatangazwa mnamo Januari 12, 2015 huko mjini Zurich .

Hatahivyo hakuna nafasi ya mshambuliaji wa Barcelona Luis Suarez ambaye alikuwa kiungo muhimu katika kuisadia timu yake ya nyumbani Uruguay kufika katika robo fainali ya michuano ya kombe la dunia nchini Brazil,lakini akasimamishwa kwa mda kushiriki katika soka yoyote kwa miezi mine kwa kumng’ata mlinzi wa Italy Giorgio Chiellini.
Previous
Next Post »