Yule Dancer wa Diamond afunguka kuhusu mimba ya Aunty ezekiel

Dansa mahiri wa staa wa muziki Bongo na nje ya nchi, Nasibu Abdul  ‘Diamond’ aitwaye Moses Iyobo, amefunguka kuwa hakuna kitu kinachompa faraja kubwa kama mimba ya mpenzi wake ambaye ni staa wa filamu Bongo, Aunty  Ezekiel.
Moses Iyobo akiwa na mpenziwe ambaye ni staa wa filamu Bongo, Aunty  Ezekiel.
Akizungumza na Amani hivi karibuni,  Iyobo ambaye nyuma kidogo alipost picha katika mtandao wa kijamii wa Instagram na kutoa pongezi kwa mpenzi wake huyo kwa kumbebea ujauzito, alisema kuwa hakuna kitu ambacho anaona fahari kama hicho.
“ Mimi tu nikiwaza mtu ambaye ninampenda kwa dhati ana mimba yangu napata faraja kubwa sana hivyo kila siku namuomba Mungu ajifungue salama na ampitishe katika majaribu mazito,” alisema Iyobo.
Previous
Next Post »