Mbona Jitihada Anazotifanya Sasa Kiongozi Mkuu Zitto, Hatukuziona Wakati Akiwa CHADEMA

Just thinking loud! 

Sasa anafanya safari juu ya safari, mikutano juu ya mikutano, facebook, twitter, kukutana na waandishi wa habari usiku wa manane, nk. Kiongozi huyu mkuu kwa sasa halali, hatulii, wala hasikii la mkuu. 

Najaribu kuvuta taswira nyuma kidogo, wakati akiwa chama kilichomlea, chama kilichomfikisha hapo alipo sikuziona jitihada hizi. Wakati huo, wenzake wakifanya mkutano Arumeru, yeye alikwenda kula bata Germany. Wakati wakiendelea na M4C, yeye alikuwa Uswizi akisaka kwa udi na uvumba majina ya waliohifadhi fedha huko. Sababu hazikuisha ilimradi tu jina na sura yake isionekane katika timu ya ukombozi.

Ninachojiuliza, kazipata wapinguvu hizi za ziada, ambazo siku chache zilizopita hakuwa nazo. Ukisoma alama za nyakati, low profile ya wakati huo na high profile ya wakati huu utajiuliza maswali na utapata hisia, hisia za usaliti. Deal lilipangwa kitambo kwa siri likabumburuka, akaenda mahakamani. Kwa sasa ni utekelezaji wa deal hilo kwa hisani ya watu wa Marekani, naamini nalo litabumburuka. 

Kama Taifa hili lingekuwa la uwazi na ukweli, na kama ofisi ya mkaguzi wa hesabu za serikali angeweza kutupia jicho, tungetaka kufahamu juu ya mapato na matumizi ya chama hiki kwa miezi mitatu tu iliyopita. Term of reference zingekuwa nini vyanzo vya mapato ya Matangazo ya moja kwa moja, safari ya kusini, na kama mapato haya yanaripiwa kodi *income tax* 

Mtu aweza kujiuliza, pamoja na madeni kwenye asasi za fedha, je ni kweli Milioni 5 zilizotangazwa kama salio la account ndizo zinagharamia mikutano na safari hizi kibao.

Democrasia inapokwa kwa watu kukubali kutumika kwa masilahi yao binafsi!

By Rpg-JF
Previous
Next Post »