Najua kuna stori nyingine huwa zinaandikwa alafu wahusika wakuu wanakuja kuziongelea baadae kwa kushangaa kilichoandikwa ambacho mara nyingi kinakua sio cha kweli.
Stori ya Wema kutopatana na ‘mama mkwe’ yaani Mama mzazi wa Diamond ni miongoni mwa stori ambazo kuna uwezekano umeshawahi kukutana nazo kwenye Magazeti au baadhi ya mitandao, stori ambazo zilianza kuandikwa tu baada ya mastaa hawa kurudi mapenzini.
Sasa kwenye exclusive na bongoclassic Wema anasema ‘Watu wanasikia vitu vingi hata kwenye Magazeti watu wanaandika vitu vingi hususani Waandishi huwa wanatengeneza ili tu kupata habari lakini hatuwezi kusema kila kitu kinachotuhusu sisi kila mtu anajua….. hapana, mbona mimi na mama tunapatana tuuuu’
ConversionConversion EmoticonEmoticon