Kila mtu ana story yake ya uhusiano wake na mpenzi wake lakini hii story ya Chris Brown na Rihanna inachukua attention ya watu wengi kutokana na mambo yanayoendelea kati yao.
Kila muda ukipita inatokea tetesi kwamba Chris Brown ana mawasiliano ya siri na Rihanna lakini bado hakukuwa na ushahidi kuthibitisha hilo.
Kitu kipya hivi sasa kinachotafsiriwa kwamba bado Chris ana mawazo na kumbukumbu juu ya uhusiano wake na Rihanna ni kutokana na picha ya rafiki wa Rihanna. Melissa Ford ambaye ni rafiki wa karibu wa Rihanna ali post picha ya Chris na Rihanna na kuandika kuwa ni hao ndio couples anaowapenda.
Baada ya hapo Chris Brown ali like hiyo picha na kuonyesha kwamba amefurahia hiyo post. Kutokana na ukaribu wa Rihanna na Melissa sio rahisi kwa Melisa ku post picha hiyo kama mambo bado ni mabaya kati ya Riri na Chris. Kama kuna lolote linaendelea kati ya Chris Brown na Rihanna lazima Melissa Ford awe anajua kwasababu wapo karibu sana.
Wachambuzi wanasema kwamba kuna kitu kinaendelea chini kwa chini kati ya Chris Brown na Rihanna na hivi karibuni kinaweza kuwekwa wazi.
ConversionConversion EmoticonEmoticon