Haya hapa ndio majibu ya Yanga kwa CECAFA baada ya kuondolewa Kagame Cup

benomarcio
Siku moja baada ya Shirikisho la vyama vya soka Afrika mashariki na kati CECAFA kuiondoa klabu ya Yanga kwenye michuano ya Kagame Cup itakayofanyika Rwanda, leo hii uongozi wa klabu ya Yanga umetoa maelezo juu ya kuondolewa kwenye michuano hiyo.
Uongozi wa klabu ya Young Africans leo umefanya mkutano na waandishi wa habari juu na kusema kilichofanywa na waandaji wa michuano ya Kombe la Vilabu Bingwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kuiondoa timu isishiriki ni cha kushangaza sana na kinadidimiza soka kwa ujumla.
Katibu Mkuu wa Young Africans Bw Beno Njovu amesema walipata barua ya mwaliko wa kushiriki mashindano tarehe 25/7/2014 na kudhibitisha kushiriki michuano hiyo kwa kuandika barua iliyokwenda TFF na kisha wao kuiwasilisha kwa CECAFA.
“Baada ya kudhibitisha kushiriki michuano hiyo tuliambiwa na CECAFA tutume orodha ya wachezaji na viongozi ambao watasafiri kuelekea nchini Rwanda kwenye michuano hiyo ili waweze kuandaa tiketi za ndege na sehemu ya malazi kitu ambacho tulitimiza” alisema Beno.
Lakini katika hali ya kushangaza jana tulipokea barua kutoka TFF ikisema CECAFA imetuondoa kwenye mashindano hayo kwa kushindwa kukidhi vigezo na kuiteua timu ya Azam kuchukua nafasi yetu “aliongeza Beno.”
Kanuni za CECAFA zipo wazi kuwa wachezaji wanaopaswa kushiriki michuano hiyo ni lazima wawe na leseni za kucheza mpira kutoka kwa chama husika, jambo ambalo ambalo orodha tuliyowapelekea wachezaji wote wataichezea Yanga msimu huu wa 2014/2015.
Kocha Marcio Maximo alianza maandalizi ya kikosi ambacho kingekwenda kushiriki michuano hiyo ambayo ilipaswa kuanza ijumaa tarehe 8/8/2014 kwa Yanga kufungua dimba la wenyeji timu ya Rayon FC .
Kikosi ambacho kocha mkuu alikichagua kwenda kwenye michuano ya Kagame kilikua na jumla ya wachezaji 20, 15 wakiwa kutoka timu ya kikosi cha wakubwa na wachezaji watano wakitoka kikosi cha pili U20 chini ya kocha Leonado Neiva ambaye amekua na wachezaji hao kwa takribani mwezi mmoja.
Lakini walichokiamua CECAFA ni kuiondoa klabu ya Yanga na kuipa nafasi timu nyingine kwa kusema kikosi kilichopelekwa hawakubaliani nacho na hata kocha mkuu Marcio Maximo haendi, hao ndo tulipojua ya kuwa wanataka majina ya watu na sio timu.
Zifuatazo ni sababu za Kiufundi ambazo Yanga ilizipelekea CECAFA kuhusu kikosi hicho kutojumuisha wachezaji wa timu za Taifa.
a) Ripoti ya kocha aliyeondoka Yanga msimu uliopita Hans ilitoa maelekezo ya kupunguza wachezaji tisa (9) na wachezaji wawili kujiunga na klabu ya Azam hivyo kufanya kikosi kupungua wachezaji 11 kutoka katika idadi ya wachezaji 30 wa msimu uliopita.
b) Wachezaji 10 wa Yanga wamekuwa na majukumu ya timu za Taifa za Tanzania (Taifa Stars), Rwanda na Uganda tangu Aprili 19, 2014 mpaka mwanzoni mwa Agosti, takribani miezi mitatu wamekuwa kambini bila kupata muda wa kupumzika.
c)  Benchi la Ufundi la Yanga ni jipya kuanzia kocha mkuu Maximo na wasaidizi wake watatu Leonardo Neiva, Salavatory Edwarda na Shadrack Nsajigwa hivyo wanahitaji muda wa kuwajua wachezaji waliokuwa kwenye timu ya Taifa ndo maana hawakuwajumuisha kwenye kikosi cha kwenda Kigali Rwanda.
d)  Baadhi ya wachezaji wanahitaji Vibali vya kufanyia kazi nchini, uhamisho wa Kimataifa (ITC) ili waweza kushiriki michuano ya Kagame, na moja ya kanuni za CECAFA mchezaji anayeshiriki mashindano hayo ni lazima awe na leseni ya kucheza mpira kwa ligi ya ndani.
e) Katika wachezaji 20 waliochaguliwa kushiriki michuano ya Kagame, wachezaji 6 wamepandishwa moja moja katika kikosi cha wakubwa msimu huu hivyo kufanya idadi ya wachezaji wa U20 kuwa watano tu.
f) Wachezaji walikokuwa kambini Taifa Stars kwa takribani miezi mitatu bila ya kupumzika, daktari alipendekeza wapate japo siku kumi na nne (14) za kupumzika ili miili yao iweze kupoa na kuanza upya tena maandalizi ya msimu mpya.
g) Yangga tunaamini hakuna mtu yoyote zaidi ya Kocha Mkuu anayeweza kutupangia kikosi cha kwanza, sababu yeye ndio anayekaa na wachezaji mda wote na kujua ubora wa wachezaji wake
Previous
Next Post »