BAADA ya kushikiliwa kwa takriban miezi tisa kwa kesi
ya madawa ya kulevya ‘unga’, hatimaye Video Queen maarufu Bongo,
Jacqueline Fitzpatrick Cliff ‘Jack Patrick’ amehukumiwa kifungo cha
miaka 6 jela huku kukiwa na uwezekano wa kupunguziwa adhabu ikawa ndogo
zaidi, Amani linaibumburua habari kamili.
Jack Patrick wakati alipokamtwa.
HUKUMU NYEPESI? Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa Jack, modo huyo alihukumiwa Jumatatu iliyopita (Agosti 11, mwaka huu) kwenye Mahakama ya Macau huko Hong Kong ambapo hukumu hiyo ilitofautiana na adhabu nyingine za madawa nchini humo ambazo huwa hukumu yake ni kunyongwa hivyo ya Jack kuonekana nyepesiii! KWA NINI NYEPESI?
Kikimwaga data, chanzo hicho makini kilidai kwamba, hukumu hiyo ya Jack ni nyepesi ukilinganisha na hukumu nyingine za madawa ya kulevya zinazotolewa nchini China ambapo hakimu alitumia muda wa dakika 27 tu kuisoma.
“Hukumu za madawa ya kulevya zinatofautiana nchini China. Kuna baadhi ya majimbo kama Beijing huwa wao ikithibitika umebeba madawa ya kulevya, unanyongwa lakini baadhi ya maeneo unafungwa miaka kadhaa. Miaka hutofautiana kulingana na sheria walizojiwekea,”
kilifunguka chanzo chetu. HUKUMU YA JACK IPOJE? Ilidaiwa kwamba, kwa mujibu wa hukumu hiyo aliyohukumiwa mrembo huyo, anaweza kupunguziwa muda wa kifungo kulingana na nidhamu atakayoionesha gerezani kama mahakama ilivyoelekeza.
Madawa aliyokamatwa nayo.
“Anaweza akapunguziwa kifungo kwa sababu hukumu imeeleza wazi kwamba anaweza kupunguziwa adhabu hiyo kama atatimiza masharti ya kinidhamu ambayo sheria za China zinamtaka atimize,” kilisema chanzo hicho.
TUJIUNGE NA CHANZO “Amehukumiwa juzi Jumatatu, ametakiwa kwenda jela miaka sita, nilikuwa nikiwasiliana naye mara kwa mara lakini juzi hiyo ndiyo kanitumia taarifa kwamba amehukumiwa na kunieleza kwamba siku hiyo aliduwaa kwa muda maana hakuamini kama anaweza kuhukumiwa kwani alikaa muda mrefu bila kujua hatima yake,” kilisema chanzo hicho kilicho karibu na Jack.
JACK AFURAHIA HUKUMU! Chanzo hicho kilizidi kumwaga data kuwa, baada ya hukumu hiyo kupitishwa, Jack alifurahia hususan kuwepo kwa kipengele cha uwezekano wa kupunguziwa kifungo kama atakidhi masharti aliyopewa na mahakama.
“Baada ya kutafakari kwa kina hukumu yake, Jack anaonekana kuifurahia kwa sababu anaamini kwake yeye itakuwa ni rahisi kutimiza masharti ya kuwa mstaarabu kadiri kipengele hicho kilivyomuelekeza,” kilisema chanzo. NDUGU HAWAJUI LOLOTE? Katika hatua nyingine, chanzo hicho kilifunguka kuwa ndugu wa Jack waliopo Bongo hawakuwa na taarifa zozote kuhusiana na hukumu hiyo.
Video queen Jack Patrick akipozi.
Kilisema kuwa kwa upande wake iliwezekana kupata haraka taarifa hizo kwani alikuwa akiwasiliana na Jack mara kwa mara kwa njia ya barua. “Ilikuwa ni rahisi mimi kunipa taarifa hizi haraka kwa sababu nilikuwa nikiwasiliana naye mara kwa mara, labda sasa hivi kwa kuwa nawapa ninyi (waandishi wetu) hizi taarifa ndiyo wanaweza na wao kujua kinachoendelea,” kilisema chanzo hicho.
NDUGU WASAKWA Wakati gazeti hili linakwenda mtamboni, lilifanya jitihada za kuwatafuta ndugu wa Jack waishio jijini Dar lakini jitihada hizo hazikuzaa matunda kwani namba zao za simu zilikuwa hazipatikani. Hata hivyo, rafiki wa karibu wa familia ya Jack ambaye hakutaka jina liandikwe gazetini alisema wamezipokea habari hizo kwa furaha kwani kulikuwa na hofu kubwa kuwa huenda ndugu yao akanyongwa.
“Ndugu, jamaa na marafiki wa karibu na Jack wameipokea hukumu hiyo kwa furaha maana walikuwa wakihofia adhabu ya kunyongwa ambayo inatolewa zaidi nchini China,” alisema rafiki huyo wa familia. JUX NAYE Ili kuzidi kujiridhisha zaidi, mapaparazi wetu walimtafuta rafiki wa karibu wa Jack ambaye alikuwa akitajwa kuwa mpenzi wake, Juma Khalid 'Jux Vuitton' lakini simu yake iliita bila kupokelewa.
TUJIKUMBUSHE Jack alikamatwa Desemba 19, mwaka jana akiwa amebeba madawa ya kulevya aina ya Heroin yenye uzito wa kilo 1.1 katika Uwanja wa Ndege wa Macau akitokea jijini Bangkok nchini Thailand kuelekea Guangzhou, Mji Mkuu wa Jimbo la Guangdong Kusini mwa China.

ConversionConversion EmoticonEmoticon