Mechi kati ya Manchester United Vs Real Madrid iliisha kwa Man United kushinda 3 – 1 dhidi ya Real Madrid kwenye uwanja wa Michigan maarufu kama The Big House. Magoli ya Manchester yalifungwa na Ashley Young (2) na Javier Hernandez (1), Gareth Bale alifunga goli pekee kwa Real Madrid kwa penati.
Story kubwa ya mechi hii sio magoli bali ni idadi ya watu walioingia uwanjani kuangalia mechi hii. Manchester United Vs Real Madrid wameweka rekodi ya kuingiiza mashabiki 109,318 na ticket zote za mechi ziliisha. Mechi hii ndio imeweka rekodi ya mechi ya soccer iliyowahi kuingiza watu mashabiki wengi kwenye viwanja vya Marekani.
ConversionConversion EmoticonEmoticon