MISS Tanga 2011, Zubeida Seif ametaka kuzichapa kavukavu na mwenzake aliyefahamika kwa jina moja la Kelly kisa kikiwa ni mkali wa wimbo wa Mwana, Ali Saleh Kiba.
Tukio hilo lililoacha watu midomo wazi lilitokea juzikati katika baa moja iliyopo maeneo ya Mwenge, Dar ambapo ubishi ulianza baada ya Zubeydah kutetea kuwa Ali Kiba anajua kuimba kuliko Nasibu Abdul ‘Diamond’ huku mwenzake akimpinga ndipo mtiti ulipoibuka.
“Wewe umezidi, unataka kusikilizwa wewe wakati ukweli unajulikana, acha hizo, ngoja nikuoneshe,” alisikika miss huyo ambaye sasa anatamba na wimbo wa Zaidi ya Wale.
Bahati nzuri watu waliokuwepo eneo hilo waliwaamulia, wakatulia.
ConversionConversion EmoticonEmoticon