MTANGAZAJI WA CLOUDS FM ATANGAZA KUJIUNGA NA CHAMA CHA ACT-TANZANIA!!!

Huyu sio mwingine ni yuleyule dada yetu anaejiita DIVA...Kupitia ukurasa wake wa INSTAGRAM ameandika kuwa kwasasa amejiunga na chama cha siasa cha ACT-Tanzania...Awali kupitia mahojiano alioyafanya siku za nyuma kwenye kituo cha redio cha Magic FM, kipindi cha Makutano na Fina Mango alisema kuwa yeye ni mwanachama wa CHADEMA..na mtu pekee ambae ni kama role mode wake ni Mbunge Zitto Kwabwe ambae DIVA alithibitisha kuwahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Mbunge huyo ambae kwasasa uanachama wake ndani ya chama cha CHADEMA upo mahakamani..na pia mbunge huyo anahusishwa shutuma za kuwa yeye na wenzake (ambao tayari walisha timuliwa CHADEMA ambao kwasasa ni viongozi waandamizi ACT) ndio wa asisi chama cha ACT-Tanzania.


Previous
Next Post »