VANESSA, JUX YADAIWA NI WAPENZI

MBONGO-Fleva anayefanya poa na ngoma yake ya Nitasubiri, Juma Mussa ‘Jux’ na staa mwenzake ambaye ana kofia nyingine ya utangazaji, Vanessa Mdee ‘V-Money’ wanadaiwa kuwa ni wapenzi, Risasi Jumatano limeinyaka.

Madai ya wawili hao kuhusishwa kimapenzi yameendelea kujidhihirisha siku hadi siku na zaidi ni hivi karibuni walipokutana kwenye ziara ya Serengeti Fiesta 2014 mkoani Kagera na Tanga, ambapo muda mwingi walionekana kugandana kama luba hadi wenzao kudai kuwa walikuwa hata wakilala chumba kimoja hotelini.
Katika kuwafuatilia, mwanahabari wetu alifanikiwa kupata baadhi ya picha za matukio yao yaliyoonesha michakato na harakati zao za kimalovee zinavyokuwa siku zote.

Mbali na Vanessa, Jux aliwahi kudaiwa kutoka na mwigizaji Jacqueline Wolper na modo Jacqueline Patrick huku Vanessa naye akiwa alisharipotiwa kutoka na Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’.
Previous
Next Post »