MSANII wa filamu Bongo, Wastara Juma, jana
alifanya uzinduzi wa aina yake wa filamu yake inayokwenda kwa jina la
Last Decision ambapo alizunguka katika mitaa mbalimbali akiinadi huku
wakazi kibao wa jiji la Dar wakijitokeza kumsapoti.
Wastara ambaye alifuatana na timu yake
iliyokuwa ikiburudisha mashabiki kwa muziki, alianza kuzindua filamu
hiyo kwa kuiuza mitaa ya Kigogo, Mbagala, Kwa Azizi-Ally na Tandika
ambapo watu kibao walijipatia nakala zao.
ConversionConversion EmoticonEmoticon