Wakati anaondoka nchini hivi karibuni, Aunt alionekana kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar, akiwa na mwanaume ambaye anadaiwa kuwa ni mume wa mtu, Moses Iyobo ‘Moze’.Baada ya habari hiyo kuripotiwa na gazeti tumbo moja na hili, Ijumaa Wikienda, Septemba 15, mwaka huu, ilidaiwa kwamba ndugu wa mumewe, Sunday hawakufurahishwa na kitendo hicho.
“Tunashangaa kumuona Aunt ameambatana na mume wa mtu na huko anakoenda pia tunasikia watakuwa wawili tu na Kassim, inatutia shaka kwa kweli,” alisema mmoja wa ndugu wa mume kwa sharti la kutoanika jina lake.
Kwa mujibu wa chanzo chetu kilichopo nchini Marekani, wawili hao walitia maguu hivi karibuni kwa mwaliko maalum wa Ubalozi wa Tanzania nchini humo ambapo Kassim alipewa nafasi mbili hivyo akaamua kumchukua Aunt.
Chanzo hicho kilizidi kumwaga data kwamba, baada ya wawili hao kufika nchini humo, walipanga katika hoteli moja kisha kuanza kujiachia kwenye viwanja tofautitofauti wakila bata ndani ya Jiji la New York.
ConversionConversion EmoticonEmoticon