MUME: KAJALA NITOE GEREZANI

Siku chache baada ya gazeti pacha la hili, Ijumaa Wikienda, toleo la Jumatatu iliyopita kuripoti juu ya utajiri mkubwa wa staa wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja ‘K’, mumewe Faraji Agustino amempigia saluti na kumuomba amtoe gerezani.


UTAJIRI WA GHAFLA
Katika msala huo, Kajala alihukumiwa miaka mitano jela au faini ya Sh. milioni 13 kwa kukutwa na hatia ya kuuza nyumba yao iliyowekwa kizuizini na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ambapo alilipiwa shilingi Milioni 13 na Wema Isaac Sepetu na sasa anapeta mtaani na utajiri wa ghafla.
Baada ya kuokolewa jela na Wema, Kajala ametembelewa na utajiri ambapo amekuwa akitanua mitaa mbalimbali ya Jiji la Dar, akisukuma magari ya kifahari, kupanga ghorofa maeneo ya Sinza-Madukani anayolipia Sh. milioni 3.2 kwa mwezi, akimiliki kampuni ya kuzalisha sinema ya Kay Entertainment huku akaunti yake ikiwa imenona kwa mamilioni kadhaa.
GEREZANI SEGEREA
Hivi karibuni, ‘mtu wetu’ alikwenda kumtembelea Faraji kwenye Gereza la Segerea, Dar ambapo alipata nafasi ya kutoa la moyoni juu ya mkewe Kajala ambaye alifunga naye ndoa kanisani miezi michache kabla ya kukutwa na msala huo.
Akizungumza kwa huruma, Faraji alisema habari za Kajala kuwa na utajiri wa kutupwa alianza kuzisikia kwa ndugu zake hivyo kumuomba staa huyo kumkumbuka kwenye ufalme wake.
amaa huyo alisema kila akikaa huwa anakumbuka good time (kipindi cha matanuzi) yao ambapo ilikuwa ni bata mwanzo mwisho hasa nyakati za wikiendi.
Kwa mujibu wa mtu wetu huyo, Faraji alimwambia: “Mwambieni K akumbuke yeye ni mke wangu. Nimemsaidia kwa mengi, asiniache nateseka huku yeye anachezea pesa ambazo anaweza kunilipia na nikatoka kifungoni. Pia akumbuke ahadi yetu ya ndoa kanisani na jinsi tulivyoishi kwa upendo.
“Bado ni mke wangu, bado nampenda sana. Nilisikia alishavua pete ya ndoa lakini ukweli ni kwamba bado mapenzi yetu yapo palepale. Kama kweli Kajala amepata utajiri naomba anitoe gerezani, sitamsahau maisha yangu yote. Kama nilivyoahidi kanisani, nitampenda na kumtunza hadi kifo kitutenganishe.”
Chanzo hicho kilidai kwamba Faraji alisema Kajala amuonee huruma, azungumze na wadau wake wote wamtoe gerezani halafu atajua jinsi ya kurejesha fedha hizo.Habari nyingine kuhusu suala hilo ilisemekana kwamba jamaa huyo ametengeneza netiweki akiwa gerezani kupitia kwa watu wake wanaomtembelea ambao wapo tayari kuungana na staa huyo ili kufanikisha jambo hilo.



 
Previous
Next Post »

ConversionConversion EmoticonEmoticon

:)
:(
=(
^_^
:D
=D
=)D
|o|
@@,
;)
:-bd
:-d
:p
:ng