BAADA YA DIAMOND KUZOMEWA JIKWAANI, HII NDIYO KAULI YA MENEJA WAKE BABU TALE

October 18 ilikua ni siku maalum ya Wakazi wa Dar es salaam kula bata kwenye msimu wa mafanikio ambao unapita mara moja kila mwaka kwenye mikoa mbalimbali ya Tanzania.
Ilikua ni good time ya ukweli sana Watanzania kumuona T.I kumuona Davido kumuona Victoria Kimani na Waje pamoja na wasanii wengine wa kimataifa ambao nao walihudhuria tamasha hili lililokuwa na watazamaji zaidi ya elfu hamsini.
Miongoni mwa wasanii waliopokelewa vizuri kwenye show hii ni pamoja na Mr Blue na Micharazo,Ally Kiba,Weusi,Vanessa Mdee,Stamina pamoja na Diamond Platnumz ambaye aliimba single 4 kwenye jukwaa hili.
Mashabiki wengi wa Ally Kiba inasemekana walipanga kuzomea wakati Diamond Platnumz anaperfoam pale jukwaani,kupitia 255 ya XXL ya Clouds Fm meneja wa Diamond Platnumz aitwae Babu Tale kaongelea hali hii.
Hizi ni sentensi 4 alizozisema.
1.Sisi tumechukulia sehemu ya mashindano,uzuri sisi tuliambiwa na uongozi wa Clouds kabla ya Diamond hajapanda ilikua saa 3 kamili tukaitwa tukaambiwa kuna watu wamejiandaa kumzomea Diamond.
2.Kama uongozi tulikaa na msanii wetu na kumjenga kisaikolojia na kumwambia kuna hivi vinatokea wao walitaka aanze Davido kisha afate Diamond kupunguza watu watakaozomea tukasema hapana pangeni show yenu kama ilivyokuwa ni sehemu ya mashabiki kufurahi.
3.Hatujaathirika kwamba msanii wetu ameshuka tunapoona watu wanapiga kelele kwa ajili yako au huna sifa ile unatakiwa uangalie umekosea wapi unaenda wapi,hatuna makosa kwa mashabiki wetu.
4.Kikubwa Diamond anafanya vizuri tunatakiwa kuhamisha macho yetu tumpigie kura Diamond kwenye tuzo za Channel O Music Awards, kwa sababu mwisho wa siku chema chajiuza kibaya chajitembeza
Previous
Next Post »