Rais
Uhuru Kenyatta wa Kenya (kushoto) akilakiwa na Makamau wa Rais, William
Ruto alipowasili JKIA leo alfajiri akitokea The Hague.
Rais Kenyatta akisalimiana na viongozi mbalimbali waliofika kumpokea leo alfajiri.
RAIS Uhuru Kenyatta wa Kenya, leo alfajiri amepokelewa kishujaa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) jijini Nairobi akitokea The Hague, Uholanzi.Rais Kenyatta alienda katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), The Hague anapokabiliwa na mashtaka ya kupanga utekelezaji wa mauaji ya kikabila yaliyopelekea kuuawa kwa zaidi ya 1,200 baada ya uchaguzi wa urais wa mwaka 2007.
Wakenya kutoka sehemu mbalimbali za taifa hilo wamekusanyika JKIA kuanzia majira ya saa 9 alfajiri kumsubiri Rais Kenyatta aliyekuwa ameambatana na mkewe Margaret Kenyatta.
Makamau wa Rais, William Ruto ndiye aliyeongoza viongozi wa serikali na kitaifa kumpokea mkuu huyo wa nchi.
Ndege iliyombeba Rais Kenyatta na viongozi alioambatana nao imetua JKIA saa 12:40 alfajiri na baadaye rais huyo alipokelewa kwa burudani za kitamaduni kutoka makundi mbalimbali ya sanaa.
ConversionConversion EmoticonEmoticon