Chris Brown Kuwahamishia Mwanae na Mama Yake Nyumbani Kwake, Anataka Kumuona Mwanae Kila Siku



Chris Brown amepanga kumchukua mwanae pamoja na mama yake na kuishi nao nyumbani kwake, mtandao wa Hollywood Life umesema.

Chris Brown, 25, anataka mwanae wa kike mwenye umri wa miezi tisa, Royalty na mama yake, Nia Amey, 31 kuhama kutoka Houston wanakoishi sasa, ili waishi naye nyumbani kwake jijini Los Angeles.

Kwa mujibu wa vyanzo vilivyoongea na mtandao huo, Chris anataka kusherehekea siku yake ya kuzaliwa kutimiza miaka 26 akiwa na Royalty.

Chris anataka kuhakikisha kuwa anamuona mwanae kila siku.
Previous
Next Post »