Mwigizaji Aliyechaguliwa Kuigiza Kwenye Filamu Ya Maisha Ya Steve Jobs.

Mwigizaji wa filamu za Bat Man Christian Bale amempiku mwigizaji mwingine maarufu Ashton Kutcher kwenye kupata nafasi yakuigiza kama Steve Jobs

Aaron Sorkin amethibitisha kuwa mwigizaji wa "Dark Knight" ametajwa kuwa mwigizaji kwenye filamu itakayohusu maisha ya msanzilishi msaidizi wa kampuni ya eletronics ya Apple.

Sorkin aliyeandika filamu ya kutengenezwa kwa Facebook "The Social Network" amesema Bale amechaguliwa sababu tunahitaji mwigizaji bora.

Filamu hii itahusu maisha ya "Steve Jobs" kama yalivyoandikwa kwenye kitabu cha Walter Isaacson ambacho Steve Jobs alikubali kiandikwe. Jobs amefariki mwaka 2011.
Previous
Next Post »