Ubavu wa Diamond, Wema Isaac Sepetu ‘Onyinye’ ndiye aliyekuwa gumzo katika sherehe hiyo baada ya watu wengi kuwa na shauku ya kuona kama atafika au la.
Wengi walitaka kujua kama atafika, ataingia kwa staili gani kutokana na minong’ono iliyokuwa ikiendelea kuwa huenda Wema asitokee kwenye sherehe hiyo kutokana na madai kuwa Diamond alikasirika baada ya kukuta mpenzi wake huyo amezawadiwa ndinga aina ya BMW 454i na Martin Kadinda hivyo kuhoji uhalali wake.
Katika hali isiyotegemewa, Diamond na Wema waliingia pamoja huku wakiwa wameshikana mikono.
Wema alivaa gauni lenye mpasuo wa aina yake, kila mmoja alimfuatilia hatua kwa hatua kutaka kujua atasababisha tukio gani.
Watu kibao waliohudhuria ukumbini hapo, walipiga shagwe za kutosha kwa Wema huku wakidai ndiye mke halali wa Diamond hivyo kumshangilia kila alipokuwa akiinuka kufanya tukio.Kwenye ukumbi huo, kila kitu kilikuwa kimeshalipiwa hivyo waalikwa wote walikunywa, kula na kucheza kwa gharama za Diamond.
Pia kulikuwa na bendi mbalimbali zilizotumbuiza hasa Ya Moto Band na wasanii mmojammoja au kundi huku kukiwa na mastaa wengi wa filamu na muziki Bongo ambao walibaki midomo wazi kutokana na namna shuguli hiyo ilivyokuwa kubwa.
Mapaparazi wetu; Shani Ramadhani, Denis Mtima, Mayasa Mariwata na Mpiga Picha Mkuu, Richard Bukos walikuwepo ukumbini hapo kuhakikisha wananasa kila tukio lililotokea na hivi ndivyo mambo yalivyokuwa;
SHILOLE, NUH FULL MAHABA
Denis: Kiongozi nawaona Shilole na Nuh Mziwanda wameongazana wanakwenda kuketi lakini hapa full mahaba au mahaba nikongorowe, kila mmoja anamdekeza mwenzake.Risasi Jumamosi: Safi, hayo ndiyo mahabati, hebu ngoja nimpe nafasi Mayasa naona anasumbua kweli.
SAA 5:45 USIKU
DIAMOND, WEMA WATINGA
Mayasa: Mkuu Diamond na ubavu wake, Wema au Madam ndiyo wanaingia kwa staili ya kumbikumbi. Pembeni yao namuona mama Diamond naye anawapa kampani. Duh! Tayari Diamond amefikia kufungua shampeni, waalikwa full kelele.
DIAMOND, WEMA WATINGA
Mayasa: Mkuu Diamond na ubavu wake, Wema au Madam ndiyo wanaingia kwa staili ya kumbikumbi. Pembeni yao namuona mama Diamond naye anawapa kampani. Duh! Tayari Diamond amefikia kufungua shampeni, waalikwa full kelele.
Hapa wasanii kibao wameanza kutoa shangwe, namuona Vincent Kigosi ‘Ray’, Elizabeth Michael ‘Lulu’, Queen Darlin, Petit Man, Chegge, Temba, Yamoto Band, Jacob Steven ‘JB’ na Aunt Ezekiel wanakula bata.
Risasi Jumamosi: Enhee…Denis: Mama Diamond naye kaingia kucheza…
SAA 7:00 USIKU KEKI YAKATWA
Bukos: Keki ndiyo inakatwa, Diamond amekata, anaanza kuwalisha wageni mbalimbali. Ameanza mama Diamond, amefuata Wema sasa.
Analishwa kwa staili ya njiwa. Anamalizia na wageni mbalimbali
wakiwemo waliozaliwa siku moja nay eye ambao siyo mastaa.Risasi
Jumamosi: Bukos muda umekwenda, yaweke matukio yote kwa pamoja utupe
uhondo mzima.Bukos: Keki ndiyo inakatwa, Diamond amekata, anaanza kuwalisha wageni mbalimbali. Ameanza mama Diamond, amefuata Wema sasa.
Baada ya nusu saa…
Bukos: Kimsingi rekodi imeandikwa. Bethidei hii watu wamekunywa, wamekula, bendi mbalimbali zimetumbuiza. Kubwa zaidi, Diamond amepewa gari aina ya BMW kama lile la Wema na menegimenti yake ya Wasafi.
ConversionConversion EmoticonEmoticon