Jibu ni hapana, Jay Z
alikuwa mmoja kati ya wageni waalikwa ambao jumla ya idadi yao walikuwa
watu mia mbili walioshiriki katika sherehe ya ndoa ya Solange jana
Novemba 16 pamoja na mastaa wengine kadhaa ikiwemo Beyonce.
Huenda ndoa ya Solange na Alan Ferguson iliyofungwa katika kanisa la Holy Trinity, New Orleans imekuwa ya kisiri kama ilivyokuwa ya Jay Z na Beyonce kwa kuwa mpaka sasa hakuna picha zilizoenea mitandaoni zikionyesha wakati wa kufungwa kwa ndoa hiyo.
Alan ni director wa video za muziki, ambapo alishawahi kufanya video za Beyonce na Jay Z kwa nyakati tofauti siku za nyuma.
Tumezoea kuona maharusi wakibebwa kwenye magari ya kifahari, ya Solange ilikuwa tofauti; Hizi ni baadhi ya picha za Solange na Alan Ferguson siku ya Jumamosi Novemba 15 wakati wa sherehe ya utangulizi siku moja kabla ya ndoa yao.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook
ConversionConversion EmoticonEmoticon