AUNTY: WANAOSEMA NIMEJIFUNGUA NI MAPEPO

STAA wa filamu Bongo, Aunty Ezekiel amewabwatukia watu waliomzushia kuwa amejifungua na kusema kuwa anawaona kama wametumwa na mapepo wabaya.
Staa wa filamu Bongo, Aunty Ezekiel.
Akizungumza na Centre Spread, Aunty alisema anawashangaa wanaokurupuka na kuzungumza kitu ambacho si cha kweli kabisa na kwamba hakuna mtu ambaye alikuwepo siku aliyopata ujauzito huo.
“ Nafikiri watakuwa na mapepo wabaya hao wanaozungumza kitu ambacho si cha kweli.  Hakuna mtu ambaye anajua nilipata ujauzito lini na nitajifungua lini, waniache kabisa,” alisema Aunty.
Previous
Next Post »