Wananchi wakiangalia jengo la
ofisi ndogo ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) la Lumumba, ambapo kilizaliwa
chama cha Tanu lililobomolewa kupisha ujenzi wa jengo jipya la chama
hicho Dar es Salaam jana
JENGO la ofisi ndogo la Chama Cha Mapinduzi (CCM)
katika Mtaa wa Lumumba Dar es Salaam ambako ndiko kilizaliwa Chama cha
Tanu limebomolewa ili kupisha ujenzi wa jengo jipya la chama hicho.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM,
Nape Nnauye alisema jengo hilo limebomolewa kwa ajili ya matengenezo ya
kawaida.
"Tunachokifanya katika jengo hili ni ukarabati wa kawaida,"alisema
Nape wakati akielezea jengo hilo ambalo limebomolewa jana kwa kutumia
tingatinga.
Kutokana na kubolewa kwa jengo hilo , viongozi wa ngazi mbalimbali
akiwemo Katibu Mkuu wa CCM,Abdulrhaman Kinana , watakuwa katika Jengo la
Umoja wa Vijana wa chama lililopo barabara ya Morogoro, wakati
ukarabati wa jengo hilo lililobomolewa ukiendelea.
Awali baadhi ya makada wa chama hicho waliokuwa eneo hilo, walidai
kuwa jengo hilo la Tanu limebolewa ili kupisha ujenzi wa jengo la kisasa
ambalo litatumika kwa ajili ya kitega uchumi.
Makada hao walisema jengo hilo litakapokamilika litakuwa la kisasa zaidi tofauti na jengo ambalo lilikuwepo eneo hilo.
ConversionConversion EmoticonEmoticon