WAKATI wagonjwa wakifa kwa
kukosa dawa hata kidonge kimoja kwenye hospitali mbalimbali nchini,
katika hali ya kushangaza, shehena kubwa ya madawa katika Hospitali
Rufaa ya Morogoro imeteketezwa kwa moto baada ya kuharibika kwa kupita
muda wake wa matumizi, Ijumaa Wikienda linakuwa la kwanza kukujuza.
Tukio hilo la aina yake lilitokea hivi karibuni mjini hapa ambapo paparazi wetu alitonywa kuhusiana na kuwepo kwa ishu hiyo ambapo alikwenda na kushuhudia lori lenye uzito wa tani 7 likisomba dawa hizo zilizoharibika kwa awamu nne mfululizo na kwenda kutupa katika dampo lililopo maeneo ya Kihonda-Viwandani.
“Ni utaratibu wetu, dawa zikiharibika huwa tunaziteketeza kwa moto,” alisema Mtei.
Tukio hilo la aina yake lilitokea hivi karibuni mjini hapa ambapo paparazi wetu alitonywa kuhusiana na kuwepo kwa ishu hiyo ambapo alikwenda na kushuhudia lori lenye uzito wa tani 7 likisomba dawa hizo zilizoharibika kwa awamu nne mfululizo na kwenda kutupa katika dampo lililopo maeneo ya Kihonda-Viwandani.
Kwenye uteketezaji huo, mwanahabari wetu
aliwashuhudia baadhi ya maafisa wa hospitali hiyo waliokuwepo kwenye
dampo hilo wakitaka tukio hilo lirushwe katika vyombo vya habari lakini
wengine wakakataa na kudai libaki kuwa siri.
Ilidaiwa kuwa baadhi ya maofisa waliokuwa wanataka jambo hilo liwe siri, walikuwa wakihofia kunyimwa dawa mpya na Bohari Kuu ya Taifa (MSD).
Ilidaiwa kuwa baadhi ya maofisa waliokuwa wanataka jambo hilo liwe siri, walikuwa wakihofia kunyimwa dawa mpya na Bohari Kuu ya Taifa (MSD).
Mwanahabari wetu alipohoji sababu za baadhi
ya maofisa hao kutaka kulificha tukio hilo, walimjia juu na kumtaka
afute picha za tukio hilo lakini jitihada zao zikagonga mwamba kwani
paparazi wetu alifanikiwa kuwatoka.
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo walihoji
kulikoni kuwe na shehena kubwa ya madawa yaliyoharibika wakati wamekuwa
wakitaabika wakiambiwa dawa hakuna mara kwa mara wanapokwenda
hospitalini hapo?
Alipotafutwa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, Godfrey
Mtei na kuhojiwa kuhusiana na tukio hilo, alikiri kutokea na kudai dawa
hizo zilikuwa zimeisha muda wake wa matumizi na hakukuwa na namna yoyote
zaidi ya kuziteketeza kwa moto.“Ni utaratibu wetu, dawa zikiharibika huwa tunaziteketeza kwa moto,” alisema Mtei.
ConversionConversion EmoticonEmoticon