Wema Sepetu Amrudisha Ujanani Bi. Mwenda

Mrembo na mwigizaji wa filamu za Kibongo, Wema Sepetu amemfanyia ‘sapraizi’ msanii mkongwe, Fatuma Makongoro ‘Bi. Mwenda’ kwa kumnunulia simu ya kisasa na kumfanya awe kama kijana.



Wema alimfanyia sapraizi hiyo hivi karibuni kwa kummpeleka Bi.Mwenda katika maduka ya Mlimani City pasipo kumwambia wanakwenda kufanya nini na alipofika, akamnunulia simu hiyo yenye uwezo wa ‘internet’.

“Namshukuru sana Wema maana sikujua tunakwenda kufanya nini Mlimani City, nikashangaa ananikabidhi simu, nimefurahi na mimi kuwa kama vijana wa kisasa, kuingia WhatsApp na Instagram,” alisema Bi. Mwenda.

Picha:Bi Mwenda akiwa katika pozi
Previous
Next Post »