Utafiti
huo uliotolewa hivi karibuni, unaonyeshsa kuwa mwanasiasa na Mbunge wa
Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe anaongoza miongoni mwa Watanzania
wanaotumia mitandao hiyo.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Tanzania ndiyo nchi pekee barani Afrika ambayo mwanasiasa kutoka kambi ya upinzani anaongoza kwa kuwa na wafuasi wengi katika mitandao ya kijamii.
Inaelezwa kuwa hiyo imetokana na ujasiri wake wa kutoa hoja za kashfa za ufisadi pamoja na ubadhirifu katika vikao mbalimbali vya Bunge katika Serikali ya Awamu ya Nne jambo linalomfanya awe mwanasiasa mwenye ushawishi mkubwa zaidi.
Mpaka wakati ripoti hiyo inatolewa, Zitto(38), alikuwa na wafuasi 219,000. Idadi hiyo imeongezeka kwa kiasi baada ya habari hizo kuandikwa na kusambazwa mtandaoni pia.
Kwa rekodi hiyo, Zitto anakuwa ndiye Mtanzania mwenye wafuasi wengi akiwazidi wasanii, wanamichezo na viongozi na wanasiasa wenzake akiwemo Rais Jakaya Kikwete ambaye akaunti yake imefungwa.
Mbunge huyo, mara nyingi hutumia mitandao ya kijamii kufikisha ujumbe kwa wananchi na wafuasi wake popote nchini na duniani kwa ujumla.

ConversionConversion EmoticonEmoticon