Wema Aendelea Kuwapa Hamasa Wanawake,Chukua Hii Kutoka Kwake

Wema Sepetu Staa mrembo kutoka Bongo Movies, Wema Sepetu  mwenye followers zaidi ya laki nne kwenye mtandao wa Instagram kwa siku za hivi karibuni ameonyesha njia kwa mastaa na watu wengine baada ya kuamua kuanza kuposti  jumbe mabalimbali zenye manufaa kwa jamii na sio majungu ambayo hayana faida yoyote, Wema amekua akiachia jumbe hizo na  huku akitumia tag mbili za BeWemaFanyaWema na 2015WalkToRemember.

Amekuwa akiandika vingi kuhamasisha wanawake kwenye kujitafutia maendeleo huu ni muendelezo tu. Baada ya hivi juzi kuwa balozi na kuzindua gari mpya ya kampuni ya Mitsubishi ASX alibandika hii.

Mwanamke simama imara. Usipojiamini mwenyewe atakuamini nani? Hamna kisichowezekana!

Huu ni mfano mzuri sana Madam tupo nyuma yako.
Previous
Next Post »