Mwanamume mmoja raia wa Hong Kong amehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa mauaji,kutawanya viungo vya nduguze ,kuwanyunyizia chumvi na kuwapika.
Mtuhumiwa huyo wa mauaji ya kushangaza ana umri wa miaka thelathini na
mmoja jina lake ni Henry Chau aliibua hisia za walio wengi katika kesi
ya namna yake mnamo 2013 wakati kichwa cha mamake mkubwa pamoja na
babake vilipobainika kuhifadhiwa katika majokofu mawili tofauti.
Majaji wa mahakama kuu nchini Hong Kong ,wakati kesi hiyo ilipokuwa
ikiendelea walisikiliza namna Chau alivyotekeleza mauaji yake ,kwanza
huua, pili hutawanya viungo vya maiti na kisha huwanyunyizia chumvi ili
kuongeza ladha ,na anasema yote hayo ni matokeo ya mapenzi yake kwa
nyama choma ya kiti moto,na nyama hiyo ya binaadamu zikisha iva ama
kuchomwa huwa anafunga nyama hizo katika makasha ya chakula paoja na
ubwabwa,na polisi walipofanya upekuzi katika nyuma yake walikuta baadhi
ya viungo katika chombo cha kuhifadhia taka.
Akitoa hukumu dhidi ya kesi hiyo,jaji Michael Stuart-Moore
alimuelezea Chau kama mbinafsi mwenye msongo wa mawazo kutokana na
mafanikio mabaya yake ya maisha na asiye na huruma kwa wengine.
Chau, alihukumiwa adhabu mara mbili kifungo cha maisha jela na miaka
tisa namiezi minne kwa makosa mawili tofauti kwa kuvunja sheria ya
kuzika miili ya familia yake isivyo kawaida kosa ambalo alikiri baadaye.
Rafiki wa Chau anayehusishwa katika mauaji hayo alikutwa hana hatia mwishoni mwa wiki iliyopita .
Taarifa za kupotea kwa wanafamilia wa Chau zilipoibuliwa ,Chau alidanganya kuwa jamaa zake walikwenda China,lakini baadaye alijisahau na kumuandikia rafikiye kupitia ujumbe mfupi wa simu kwamba aliwaua jamaa zake.
Chau mwenyewe hujiita mwendawazimu katika ujumbe aliokuwa akiwatumia
watu wake wa karibu na kusema kwamba hawezi kumuonea huruma mtu yeyote
kutokana na maumivu aliyopitia wakati wa makuzi yake utotoni mpaka
anakuwa mtu mzima.Na alimua kuwadanganya polisi ilia pate wasaa wa
kuwaaga marafiki zake.
ConversionConversion EmoticonEmoticon