WOLEPR ALEWA AZIMA, WEMA SEPETU NA MWANAUME SHOGA PATASHIKA!

Masistaduu wawili kunako gemu la Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu na Jacqueline Wolper Massawe wakipiga mtungi usiku mnene. ENEO LA TUKIO Hatari! Masistaduu wawili kunako gemu la Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu na Jacqueline Wolper Massawe, wamejikuta wakipiga ulabu hadi kulewa chakari, kisa kikielezwa kwamba wana msongo wa mawazo, Risasi Jumamosi linafunguka.
Tukio hilo lililoshuhudiwa na gazeti hili lilijiri hivi karibuni, usiku mnene kwenye pati ya kuzaliwa (birthday) ya meneja wa kampuni ya Wema ya Endless Fame almaarufu Petit Man iliyofanyika kwenye nyumba ya jamaa mmoja maeneo ya Kinondoni-Manyanya jijini Dar na kuhudhuriwa na mastaa kibao.


Katika pati hiyo ambayo mbali na mastaa ilihudhuriwa na watoto wa mjini, watu waligonga msosi wa kufa mtu kisha vikafuata vinywaji.
Tofauti na ‘maraia’ wengine, Wema na Wolper walikuwa wakigonga vinywaji vikali hadi wakawa tilalila na kuanza kufanya vituko, jambo ambalo liliwashangaza wengi.Kadiri muda ulivyokuwa unasonga ndivyo mastaa hao walivyozidi kucharuka tofauti na walipofika kwani walionekana wapole na wastaarabu kupita maelezo.
Previous
Next Post »