Baada ya Mwaka Moja, Leo Monalisa Atoboa Mazito Kuhusu Kilichotokea Kwenye Msiba wa George Tyson

Leo ikiwa ni mwaka mmoja toka aliekuwa muongozaji wa filamu na vipindi vya TV hapa Bongo, George Tyson kufariki dunia, mwigizaji  Yvonne Cherrie ‘Monalisa’ ambaye alizaa na marehemu  afunguaka mazuto kupitia ukurasa wake mtandaoni.

Mara baada ya kubandika picha hiyo hapo juu monalisa akiwa na marehemu Tyson na mtoto wao, monalisa aliandika;

Wiki 78 zilizopita @jojityson alipost hii pic na kuandika
My family @monalisatz @soniamonalisa

Leo ni mwaka mmoja toka uondoke George..bado ni ngumu sana kwetu.Ulipoondoka mengi huku nyuma yamesemwa kama unavyowajua wabongo kwa kuongea,wengine waliniporomoshea matusi eti najishaua nalia nini?mmh!wabongo bana.wanaojifanya ndugu zako eti nao wakaanza kukimbilia mali,bila hata kujua zilitoka wapi,umezipataje..kweli nilikuwa naonaga hivi vitu kwenye muvi ila bwana yametokea baada ya ww kuondoka.Ila nakushukuru sana sehemu ulizoandika mwenyewe ulimkumbuka sana Sonia na Eugene,watoto ambao mm nawafahamu.Mali zingine hadi leo watu wamesepa nazo ila tumeamua kuwaachia maana ni mali tu zinapita.Sonia is doing good shuleni japo mwanzoni alikuwa anatoka nje na kulia peke yake,ss hv amemove on na bado pia anasoma shule ya music na siku ya kuagwa kwako alikuahidi she ll never stop singing for you...nitarudi kukupa story zingine maana najua mwaka mmoja ni mwingi na umepitwa na mengi japo naamini kwamba Umepumzika kwa Amani...George

Monalisa akaadika tena

Eti leo nasikia kuna ibada ya kukuombea.Duh!hii kali nimeisikia kwenye social media tu.walivyoona wameharibu naanza kutumiwa sms kwa fujo.Mmh!tunashukuru wanakukumbuka hata kukuombea lakini isiwe tu ni namna nyengine ya kujipatia ela.Maana siku ya kuagwa kwako pale Leaders Club watu waliombwa kutoa sadaka kwa ajili ya watoto ila ziliishia tumboni mwa wanaojua kula ela..wengine waliahidi kwa jinsi ulivyowasaidia wangemsaidia Sonia..loh!ilikuwa ni gia ya kuondokea hakuna mtu aliyemsaidia narudia HAKUNA.si ndugu zako,si rafiki nasema HAKUNA.
Nitarudi tena George..nina mambo mengi ya kukueleza..Pumzika kwa amani
Previous
Next Post »