Umati wa watu wakishuhudia ajali hiyo ilivyotokea. Kikosi cha uokoaji wakitathimini namna ambavyo ajali hiyo ilivyotokea na kuharibu majengo. Shughuli za uokoaji zikiendelea eneo katika la tukio.
Maofisa wa Jeshi la nchi hiyo wamesema kuwa, tayari miili 20 ya watu waliokufa kwa ajali hiyo imepatikana katika eneo la ajali.
Maofisa hao wameongeza kuwa, ndege hiyo ya uchukuzi ya Majeshi ya taifa hilo, ilianguka muda mfupi baada ya kupaa angani.
Ndege hiyo ya kubeba mizigo aina ya C-130 Hercules ilikuwa na wahudumu 12 na abiria 50 wakati ilipoanguka.
Kuna ripoti kuwa watu bado wanasikika wakipiga mayowe katika majengo yaliyoanguka.
Ndege hiyo iliharibu kabisa nyumba ambayo iliangukia katika mji wa Medan, kaskazini mwa jimbo la Sumatra.
Picha za runinga zilizorekodiwa wakati ndege hiyo ilipokuwa ikianguka na zile za kwenye mitandao ya kijamii zinaonesha moto unatoka kwenye mabaki ya ndege hiyo.
Msemaji wa Jeshi la Anga nchini Indonesia amesema kuwa, rubani alikuwa ameomba kurejea katika uwanja wa kambi ya kijeshi kwa sababu ya matatizo ya kimitambo.
CREDIT: BBC
JAKARTA, Indonesia
Ndege ya uchukuzi ya Jeshi la Anga la nchini Indonesia imeanguka eneo la Medan, Kaskazini mwa jimbo la Sumatra mapema leo.Maofisa wa Jeshi la nchi hiyo wamesema kuwa, tayari miili 20 ya watu waliokufa kwa ajali hiyo imepatikana katika eneo la ajali.
Maofisa hao wameongeza kuwa, ndege hiyo ya uchukuzi ya Majeshi ya taifa hilo, ilianguka muda mfupi baada ya kupaa angani.
Ndege hiyo ya kubeba mizigo aina ya C-130 Hercules ilikuwa na wahudumu 12 na abiria 50 wakati ilipoanguka.
Kuna ripoti kuwa watu bado wanasikika wakipiga mayowe katika majengo yaliyoanguka.
Ndege hiyo iliharibu kabisa nyumba ambayo iliangukia katika mji wa Medan, kaskazini mwa jimbo la Sumatra.
Picha za runinga zilizorekodiwa wakati ndege hiyo ilipokuwa ikianguka na zile za kwenye mitandao ya kijamii zinaonesha moto unatoka kwenye mabaki ya ndege hiyo.
Msemaji wa Jeshi la Anga nchini Indonesia amesema kuwa, rubani alikuwa ameomba kurejea katika uwanja wa kambi ya kijeshi kwa sababu ya matatizo ya kimitambo.
CREDIT: BBC
ConversionConversion EmoticonEmoticon