icha ya kuwa headlines za soka duniani kote ilikuwa ni mchezo wa El Clasico kati ya Real Madrid dhidi ya FC Barcelona katika uwanja wa Santiago Bernabeu, nchini Uingereza kulikuwa na mchezo mmoja uliyokuwa unavuta hisia za watu wapenzi wengi wa Ligi Kuu Uingereza.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana nasi Kwa habari Zaidi.
Uingereza ulipigwa mchezo kati ya Manchester City dhidi ya klabu ya Liverpool katika uwanja wa nyumbani wa Man City Etihad, mchezo kati ya Man City dhidi ya Liverpool ulimalizika kwa Liverpool kuibuka na ushindi wa jumla ya goli 4-1 na kuifanya Man City kushuka kileleni mwa Ligi Kuu Uingereza na kushika nafasi ya tatu nyuma ya Leceister City wanaoongoza Ligi kwa sasa kwa point 28 na Man United wakiwa nafasi ya pili kwa kuwa na point 27.
Liverpool walianza kupata goli la kwanza dakika ya 8 baada ya mchezaji wa Man City Eliaquim Mangala kujifunga, goli la pili la Liverpool lilifungwa na Philippe Coutinho dakika ya 23 wakati goli la tatu lilifungwa na Roberto Firmino dakika ya 32 kabla ya Martin Skirtel kuhitimisha kwa kufunga goli la nne dakika ya 81 huku Man City wakiambulia goli moja la kufutia machozi lililofungwa na Sergio Aguero dakika ya 44.
Video ya magoli yote mtu wangu hii hapa
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana nasi Kwa habari Zaidi.
ConversionConversion EmoticonEmoticon