Mahakama Kuu kutoa uamuzi kesi ya Mbowe Septemba 23

September 23, 2021 ndio tarehe ambayo Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam inatarajiwa kutoa uamuzi wa mapingamizi manne yaliyowasilishwa na upande wa Jamhuri katika kesi namba 21/2021 iliyofunguliwa na Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe dhidi Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mkurugenzi wa Mashitaka na IGP. Miongoni mwa mapingamizi ni kutaka kesi hiyo iondolewe Mahakamani kwa kuwa utaratibu uliotumika kufungua kesi hiyo umekiuka sheria huku wakiomba mapingamizi hayo yasikilizwe kwa maandishi mbele ya Jaji John Mgeta. Mapingamizi hayo yamewasilishwa na Wakili Mkuu wa Serikali Hangi Chang’e huku upande wa Mbowe ukiwakilishwa na Jopo la Mawakili Saba wakiongozwa na Peter Kibatala ambao wamesema hawana pingamizi na hoja za Serikali. Baada ya kutoa hoja hiyo, Jaji Mgeta akatoa utaratibu wa namna pande zote mbili kuwasilisha hoja zao ambapo Pande zote zinatakiwa kuwasilisha hoja Septemba 6, 9 na 13, 2021.
Previous
Next Post »