Rais Museveni atoa onyo kwa magaidi baada ya mlipuko kutokea Kampala

Rais Yoweri Museveni wa Uganda ambaye pia ni amiri jeshi mkuu amesema watawashughulikia magaidi wote wanaojaribu kuishambulia Uganda. Hii ni baada ya watu ambao hawajulikani, walitega bomu jana usiku kwenye sehemu moja ya starehe yani 'Bar' ijulikanayo kwa jina la Digida eneo ambalo watu wanapokula nyama ya Nguruwe, kitongoji cha Komambogo, mjini Kampala. Katika taarifa iliyotolewa na Rais Museveni kwenye mtandao wake amesema amefahamishwa na vikosi vya usalama kuwa watu watatu walikwenda kwenye bar hiyo na kuacha mfuko wa plastiki chini ya meza waliokuwa wamekaa, na baadaye kulipuka na kuua mtu mmoja na wengine watano kujeruiwa. Museveni amesema ni kundi la magaidi lakini watawakamata wote na kutokomeza harakati zao. Hivi karibuni serikali ya Uingereza ilitaadharisha Uganda kushambuliwa na magaidi, lakini tahadhali hiyo haikuelezea magaidi wanakwenda kushambulia wapi. Pia serikali ya Ufaransa ilionya raia wake nchini Uganda kuacha kwenda sehemu za umma, kama vile bar, sehemu za Ibada, usafiri wa umma na sehemu zinazopendwa na wageni kwa ajili ya usalama wao. Msemaji wa jeshi la polisi nchini Uganda Fred Enanga amesema jeshi la polisi wakishirikiana na vikosi vingine vya usalama wanaendelea na uchuguzi kuwatafuta waliohusika na shambulio hilo.
Inakumbukwa kuwa mwaka 2010 Uganda ilishambuliwa na magaidi wa Al Shababu wakati watu wakiangalia fainali ya kombe la dunia na kuua zaidi ya watu 70 kwenye uwanja wa raga wa Kyadondo na mgahawa wa Ethiopia Kabalagala. Kuanzia hapo Uganda imekuwa katika hali ya tahadhali ya vitendo vya magaidi. Ila watu wanahoji saa hizo zilikuwa za marufuku ya kutoka nje ,, inakuwaje watu walikuwa wanakunywa pombe kwenye bar huku bar nyingine zikiwa zimefungwa kwasababu ya marufuku iliyokuepo tangu Machi mwaka jana 2020 kutokana na janga la uviko19.
Previous
Next Post »