Ubalozi wa Uingereza Kenya watoa taarifa ya mauaji ya Agness Wanjiru

Ubalozi wa Uingereza nchini Kenya umetoa taarifa kuhusu mauaji ya kutisha ya bi Agnes Wanjiru yaliyotokea mwaka 2012 . Balozi wa Uingereza nchini Kenya bi. Jane Marriott ameandika kwenye kurasa ya twitter kwa kueleza masikitiko yake kwa familia ya Agnes na kuhakikishia Wakenya kuwa Uingereza itashirikiana na Kenya katika uchunguzi na kusaidia kukabiliana na tatizo hilo ipasavyo. ""Mnamo mwaka 2012, Uchunguzi maalum ulifanyika nchini Kenya dhidi ya askari wa Uingereza ambao wanafanya mazoezi nchini Kenya baada ya polisi kuomba na hakuna maombi zaidi yaliyopokelewa wakati huo. "Baada ya uchunguzi kumalizika mwaka 2019, tulielewa kuwa mamlaka ya Kenya inafuatilia mauji hayo. Tutashirikiana na polisi wa Kenya kufanya uchunguzi. ""Mwenendo wa jeshi la Uingereza hapa ni muhimu sana kwetu. Wanafanya mengi mazuri huko Nanyuki, katika uchumi na jamii. Lakini ambapo kuna maswala yanayoenda kinyume, tunayo na tunayashughulikia "Wakuu wa jeshi kutoka Uingereza wanakuja mara kwa mara , na watakuja wiki chache zijazo kujadili kuhusu mauaji ya bi.Wanjiru na kushirikiana na Kenya katika uchunguzi. Taarifa iliyoandikwa katika Sunday Times nchini Uingereza Jumapili, Oktoba 24, inaonesha kwamba kuibuka kwa taarifa hiyo kumekuja baada ya wanajeshi wanne kubainisha kuwa afisa anayeshukiwa aliwaambia juu ya upangaji huo na kuwaonesha mwili. Askari hao ambao hawajatajwa majina yao , wameeleza kuwa mwaka 2012, mshukiwa na wafanyakazi wenzake walienda bar katika eneo la Nanyuki ambapo wanajeshi walikuwa wanafanya mazoezi. Wakati wapo bar , aliwaambia wenzake kuwa amemuua mwanamke mmoja na kuwapeleka eneo ambalo mwili wa mwanamke huyo ulipatikana. Watoa taarifa hao wa siri walisema juu ya majaribio yao ya kueleza suala hilo kwa wakuu wao bila mafanikio kwa kuwa wakuu walikuwa wanataka kudumisha uhusiano wa Kenya na wanajeshi wa Uingereza kuendelea kufanya mazoezi katika viwanja vya Nanyuki. Kesi hiyo haikupata hitimisho kwa miaka tisa sasa, ikimuhusisha mwanamke mwenye miaka 21 ambaye walidai kuwa kahaba ambay alikuwa ana mtoto wa miezi mitano wakati huo. Taarifa zilionesha kuwa alionekana mara ya mwisho akiwa na askari huyo wa Uingereza. Mashaidi wanasema wakuu wa kikosi walijaribu kutoeleza ukweli juu ya tukio hilo , ambapo mwili wa marehemu ulipatikana baada ya miezi miwili tangu auawe.
Hata hivyo hivi karibuni, mnamo Septemba 24 mwaka huu kuna wakazi wa Kenya ambao waliwapeleka wanajeshi wa Uingereza mahakamani wakitaka kulipa fidia baada ya askari hao kuunguza eneo la msitu. Taasisi ya FOI imebainisha kuwa vikosi vya jeshi la Uingereza vilivyokuwa nchini Kenya vilisababisha matukio matano ya moto mwaka huu ambayo hayakuripotiwa, imeeleza tovuti ya Declassified UK, inayochambua habari za sera ya nje ya Uingereza. Hatua hiyo imekuja siku kadhaa kabla ya Wizara ya Ulinzi ya Uingereza haijajiandaa kujitetea dhidi ya madai ya fidia yaliyotolewa na jamii katikati ya Kenya, ambayo yamesema vikosi vya Uingereza vilichoma ekari 12,000 za hifadhi ya wanyama pori kwa bahati mbaya wakati wa mazoezi mwezi Machi. Mwanajeshi mmoja wa Uingereza anadaiwa aliandika ujumbe wa Snapchat kuhusu moto katika hifadhi ya Lolldaiga: "Miezi miwili nchini Kenya baadaye na tumebakiza siku nane tu. imekuwa vyema, tukasababisha moto, tukamuua tembo na tukajisikia vibaya lakini.....'' Tovuti hiyo imeorodhesha matukio yaliyopita ya moto karibu na Mlima Kenya kama ifuatavyo; Tarehe 24 Februari: Moto uliwaka kwenye ranchi ya Ole Maisor eneo la mita 200 kwa 500 liliungua. Tarehe 27 Februari: Moto uliwaka katika ranchi ya Mpala na kuunguza eneo la chini ya mita 200 kwa 200''. Tarehe 28 Februari: Moto katika kituo cha Archers na kuunguza eneo la chini ya mita 200 kwa 200. Tarehe 1 Machi: Moto katika eneo la Ol Doinyo Lemboro Tarehe 1 Machi: Moto kwenye ranchi ya Ole Maisor Hakuna tukio lolote la moto lililochunguzwa, tovuti hiyo imeeleza. Imenukuu Wizara ya Ulinzi ikisema "ilihitajika tu kuchunguza moto mkubwa wakati upoteaji wa vifaa, majeruhi au uharibifu mkubwa wa mazingira umetokea". "Hakuna nyaraka zilizoshikiliwa" kuhusu matukio mengine mawili ya moto ambayo Jeshi la Uingereza lilikiri kusababisha mnamo 2019, kwa sababu inasema "hawakufikia kiwango cha kufanyika uchunguzi". moto
Mwaka 2015, Uingereza imetia saini mkataba wa makubaliano ya kuendelea kuwa na kambi yake ya majeshi nchini Kenya kwa muda wa miaka mitano zaidi. Mkataba huo mpya umeiruhusu Kenya kuwashtaki na kuwafunga wanajeshi wa Uingereza wanaovunja sheria za nchi hiyo ya Afrika Mashariki. Suala hilo la kuwachukulia hatua wanajeshi wa Uingereza lilitishia kuvunja uhusiano baina ya nchi hizo mbili. Baada ya majadiliano makali Uingereza umekubali wanajeshi wake wanaovunja sheria wakiwa nchini Kenya kushitakiwa. CC BBC SWAHILI
Previous
Next Post »