Tuzo ya mwimbaji bora wa kike Afrika Mashariki, Lady Jay Dee
Mwimbaji bora wa kike Afrika Mashariki, Lady Jay Dee.
Lady Jay Dee ameipokea tuzo ya AFRIMMA ya mwimbaji bora wa kike Afrika Mashariki siku mbili baada ya kutangazwa mshindi wa tuzo hiyo.
Baada ya kuishika mkononi tuzo hiyo ambayo inakuwa tuzo yake ya 30, Jide 'Commando' amewashukuru mashabiki wake kwa ushiriano waliouonesha kwake.
“Tuzo yangu ya 30. Asanteni kwa ushirikiano, nimeipokea na ninarudi nayo nyumbani. Shhhhhh! !!! Kimya Kimya.” Ameandika Lady Jay Dee kwenye ukurasa wake wa Facebook na kupost picha ya tuzo hiyo..!!!!
ConversionConversion EmoticonEmoticon