ALI KIBA VS DIAMOND WANAGOMBEA UFALME..!!


INAWEZEKANA lisiwe jibu sahihi lakini kwa kiasi fulani linatoa picha juu ya kinachoendelea kwenye ulimwengu wa Bongo Fleva, kila kona gumzo ni juu ya nani mkali kimuziki kati ya Diamond Platnumz dhidi ya Ali Kiba.

Alikiba na mpenzi wake kwa picha wakipoz..!
Nasibu Abdul ‘Diamond’ ndiye staa kwa sasa na amedumu kileleni kwa miaka kadhaa, hilo halina ubishi, lakini Ali Kiba amerejea kwa kutoa nyimbo mbili za Kimasomaso na Mwana baada ya ukimya wa miaka kadhaa, ukijumlisha vijembe ambavyo wanapigana wawili hao kwenye vyombo vya habari, gumzo limekuwa kubwa juu ya nani ni mkali kati yao kimuziki.
Vs 
Ali Kiba ambaye anatarajiwa kufanya shoo yake ya kwanza kubwa tangu aliporejea, katika Tamasha la Matumaini kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, Agosti 8, 2014, ameonekana kuongoza kwenye kura za maoni juu ya nani mkali kati yake na Diamond kupitia kuraza za mitandao ya kijamii zikiwemo Twitter na Facebook.

Previous
Next Post »