MAKUBWA! Mambo yamekuwa mambo, kadi ya gari jipya la
staa wa sinema za Bongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ imeibua
mazito kufuatia Jeshi la Polisi Dar es Salaam kubaini kuwa namba ya
Sanduku La Posta (SLP) iliyoandikwa kwenye kadi hiyo ni Wizara ya Mambo
ya Ndani Tanzania.
IMEVUJAJE?!
Hilo lilibainika baada ya gazeti dada na hili, Ijumaa toleo la Ijumaa iliyopita kuandika habari yenye kichwa kisemacho; LULU AANDIKA HISTORIA.
Katika habari hiyo, Lulu alipewa shavu kwa vile alinunua gari aina ya Toyota Rav 4 New Model kwa pesa zake mwenyewe tofauti na baadhi ya mastaa wa Bongo ambao huhongwa magari na wanaume
Kadi ya gari la ‘Lulu’ yenye anuani za jeshi la Polisi (S.L.P ya 9140).
POLISI NAO WANENA
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, ambako ndiko usajili wa gari hili ulifanyika katika ofisi za TRA, Zakaria Sebastian, alisema jeshi lake halina taarifa za kuwepo kwa jambo hilo lakini watalifuatilia kwa karibu.
“Huenda ni mke wa askari au mwanafamilia. Unajua kuna baadhi ya maofisa wana msamaha, huenda alitumia hivyo, lakini tutafuatilia,” alisema kamanda huyo ambaye alielezwa kuwa, Lulu hajawahi kuwa mke wala mwanafamilia ya mwajiriwa wa jeshi la polisi.
“Kama hajawahi kuwa mwenye kustahili kutumia anuani hii, basi tutafuatilia ili kujua wakati akiitumia, je alikuwa anakusudia kufanya jinai? Tukijiridhisha hivyo bila shaka sheria itafuata mkondo wake.”
UCHUNGUZI WA RISASI MCHANGANYIKO
Katika uchunguzi wa gazeti hili, anuani hiyo imeshatumika na Jeshi la Polisi Magomeni na Mkoa wa Polisi wa Ilala jijini Dar. Namba hiyo inatofautiana tarakimu moja na ya Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam.

ConversionConversion EmoticonEmoticon