Taarifa ya Wizara ya Afya kuhusu ugonjwa wa Ebola kuingia Tanzania.

Ugonjwa wa Ebola ambao kwa sasa umeingia kwenye headline ya vyombo mbalimbali vya habari kutokana kwenye nchi mbalimbali barani Afrika kuna taarifa zimetoka zinasema kuwa ugonjwa huo tayari umeingia Tanzania. Waziri wa Afya wa Tanzania Seif Rashid amesema kuwa wagonjwa hao waliohisiwa kupata maambukizo hayo kutokana na dalili za awali ni wa kutoka Benin na Mtanzania,lakini baada ya vipimo wameonekana hawana maambukizo hayo.
Waziri Seif Rashid amesema kuwa tayari eneo maalumu limetengwa kwa ajili ya kufanyia uchunguzi wagonjwa wanaotiliwa shaka kuwa na ugonjwa huo,Kauli hiyo imekuja baada ya kufanyiwa uchunguzi kwa wagonjwa wawili waliohisiwa kuwa na ugonjwa huo.
Vifaa maalumu vitakavyotumiwa na watoa huduma katika kuhudumia wagonjwa, vimewekwa pia,Wizara ya Afya pia imeongeza uwezo wa kufanya uchunguzi,katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere,ambao wasafiri wengi kutoka nje huutumia.
Ebola_Virus_Victim
Previous
Next Post »