Martin Lawrence na Will Smith ndio mastaa wa movie hizi mbili ambazo zina action na comedy ndani yake. Kama wewe ni mpenzi wa hizi movie basi taarifa ikufikie kwamba Bad Boys 3 ipo kwenye maandalizi.
Akiwa kwenye interview ya TV show actor Martin Lawrence aliulizwa kuhusu plan za movie ya Bad Boys 3 ambayo imekuwa kwenye tetesi kwa muda mrefu na Martin alijibu,”Nimeongea na director jana tu na ameniambia wanafanyia kazi script hivi sasa na wanakaribia kuimaliza. Hivi karibuni mtapata taarifa rasmi ”
Martin hakuthibitisha uhusika wa star mwenzake Will Smith kwenye hiyo movie kwasababu ni bado mapema sana.
ConversionConversion EmoticonEmoticon