YEMI ALADE KUTUA BONGO LEO


Hayawi hayawi sasa yamekuwa! Mkali wa ngoma ya Johnny, Yemi Alade, hatimaye anatarajiwa kutua Bongo saa tano usiku, leo Jumanne, Agosti 5, 2014 tayari kwa kukinukisha kwenye Tamasha la Usiku wa Matumaini ambalo limebakiza siku chache kabla ya kutimua vumbi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Agosti 8, 2014.

Mkali wa ngoma ya Johnny kutoka nchini Nigeria, Yemi Alade.
Akipiga stori na Showbiz, mratibu wa tamasha hilo, Luqman Maloto alisema Alade anatarajiwa kutua kwa ndege ya Shirika la Kenya Airways akitokea Lagos, Nigeria na kuwataka mashabiki wa mwanamuziki huyo, kujitokeza kwa wingi kumpokea katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere.
“Kama tulivyowaahidi kwamba mwaka huu kwenye Tamasha la Usiku wa Matumaini tunamdondosha Yemi Alade, mwanamuziki huyo atatua leo usiku tayari kwa kazi iliyomleta Bongo, kuzikonga nyoyo za mashabiki watakaohudhuria kwenye Tamasha la Usiku wa Matumaini na kumtafuta Johnny wake,” alisema Maloto.
Katika tamasha hilo, mbali na burudani ya nguvu kutoka kwa Yemi Alade, pia Ali Kiba atakamua shoo ya nguvu sambamba na wasanii wengine kibao wa Bongo wakiwemo Navy Kenzo (Nahreel na Aika), Zuwena Mohamed ‘Shilole’, Madee, R.O.M.A Mkatoliki, Meninah, Juma Nature na kundi zima la Wanaume Halisi, mshindi wa Shindano la Amani Talent Search, Paschal Dominick ‘P-Plan’ na Scorpion Girls (Jini Kabula na Isabela).
John de bad guy 
Previous
Next Post »