MCHUMBA WA SHILOLE AKATALIWA UKWENI

OHOOO! Mchumba wa staa wa Mduara Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shishi Baby’, Naftari Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ amejikuta katika wakati mgumu baada ya kukataliwa ‘ukweni’ kwao, Tabora
Tukio hilo lilijiri ndani ya Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi mjini hapa wakati wawili hao walipokuwa wakipafomu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta ndipo mashabiki waliposema hawamkubali Nuh na badala yake aolewe na DJ Zirro.
Wakati shoo ya wawili hao ikiendelea, Shilole alikatisha muziki kwa muda na kuwaambia mashabiki kupitia kipaza sauti wamwambie kama Nuh Mziwanda ana vigezo vya kuwa mumewe ndipo wakasema hapana na kumpendekeza DJ Zirro ambaye alikuwa akipiga muziki kwenye shoo hiyo.
“Kusema kweli kuna muda nimejisikia vibaya ingawa hapohapo jukwaani nilijifikiria na kugundua kuwa ni gemu tu hivyo nimejifariji kwa kuona kama ni sehemu ya burudani tu,” alisema Nuh Mziwanda.
Previous
Next Post »

ConversionConversion EmoticonEmoticon

:)
:(
=(
^_^
:D
=D
=)D
|o|
@@,
;)
:-bd
:-d
:p
:ng