ODAMA LAIVU NA MUME WA MTU

MSANII nyota wa filamu za kibongo, Jennifer Kyaka maarufu kwa jina la kisanii kama Odama, usiku wa kuamkia Jumapili iliyopita alinaswa Live akiwa kwenye pozi la aina yake akiwa na pedeshee maarufu jijini Dar anayefahamika kama Papaa Daudi ambaye anadaiwa kuwa mume wa mtu.
Wawili hao walinaswa wakiwa kwenye pozi hilo ndani ya Ukumbi wa Ten Lounge uliopo Makumbusho jijini Dar es Salaam ambapo Odama alikuwa akimdekea mwanaume huyo kama mtu wake wa karibu.
Wakiwa ukumbini humo, wawili hao walionekana kupata kiburudisho kwa namna yake huku mara kwa mara wakigonga ‘chiaz’ na kunyweshana mvinyo na kuwafanya waliokuwa karibu yao kuwaonea gere.
Licha ya macho ya watu kuonekana kuwatazama kwa muda mwingi, lakini wawili hao hawakumjali mtu bali waliendelea kuponda raha huku mikono ya mwanaume ikiwa haichezi mbali mapajani mwa Odama.
Baada ya kupata picha kadhaa za wawili hao, Paparazi wetu aliwasogelea na kuwauliza kama wao ni mtu na mwenza wake, lakini wakabeza na kumtaka awaache wale raha zao.
Aaaah jamani hebu tuacheni jamani nyinyi kila mkiona watu wanastarehe, mnaanza kuhisi ni wapenzi, hebu tuacheni jamani,” aliongea Odama huku akipata mvinyo.Papaa Daudi alipotakiwa kutoa neno, alisema:  “Nakuomba sana, we ndugu mwandishi, ntafute siku nyingine leo hatuna muda.”
Previous
Next Post »